BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMAMOSI TAREHE 18-01-2020

Manchester United inakaribia kufikia makubaliano na Sporting Lisbon kumsaini kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes , 25 katika mkataba unaoweza kuwa na thamani ya £60m lakini uhamisho huo hautafanyika kwa haraka.. (Sky Sports)
Wakati huohuo , Manchester United pia wanajaribu kumsajili kiungo wa kati kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Manchester Evening News)
Kiungo huyo anaweza kinda wa klabu ya Birmingham City Jude Bellingham , baada Manchester United kuwasilisha ombi la £25m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 16. (Daily Record)
Newcastle United inatarajiwa kuwasilisha ombi la kumnunua mshambuliaji wa Hull City na England Jarrod Bowen ,23, baada ya meneja Steve Bruce kuhakikishiwa na mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley kwamba atamuunga mkono katika dirisha doho la uhamisho wiki hii.. (Telegraph)

Mchezaji wa Ivory Coast Eric BaillyHaki miliki ya picha

Manchester United pia ina mopango wa kumuongezea kandarasi yake beki wa Ivory Coast Eric Bailly' ili kumzuia katika klabu hiyo hadi 2022. (ESPN)
Inter Milan inakaribia kumsaini winga wa Chelsea Victor Moses, 29, baada ya mkufunzi Antonio Conte kuwasilisha ombi maalum kwa klabu hiyo ili kumsaini mchezaji huyo wa Nigeria, ambaye kwa sasa anahudumu kwa mkopo katika klabu ya Uturuki Fenerbahce. (Daily Mail)
Beki wa kushoto wa Paris St-Germain Layvin Kurzawa, 27, ametoa ishara kwamba anakaribia kujiunga na Arsenal mwezi huu baada ya kutangaza kwamba amejiunga na ajenti mmoja wa Uingereza. agency. (Evening Standard)

Layvin Kurzawa

Arsenal wamekubali mkataba wa miaka mitano na Kurzawa, huku beki huyo akitarajiwa kuondoka PSG mwisho wa msimu. (Express)
Wakati huohuo , Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Arsenal Edu amepanga mazungumzo na klabu ya Athletico Paranaense kuhusu mchezaji wao wa Brazil mwenye umri wa miaka 22 Bruno Guimaraes. (Goal via Mirror).
Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 27, anakaribia kuelekea Inter Milan baada ya kufanikisha mazungumzo na klabu yake ya. (Sun)

Christian EriksenHaki miliki ya picha

Klabu ya Los Angeles Galaxy imemsaini mshambuliaji Javier "Chicharito" Hernandez, 31, kutoka Sevilla kwa kandarasi itakayomfayan mchezaji hyo kuwa mchezaji anayelipwa kitita kikubwa zaidi katika ligi hiyo ya soka nchini Marekani. (Sports Illustrated)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Emre Can, 26, huenda akaelekea AC Milan kutoka Juventus. (Sportmediaset - in Italian)
Mshambuiaji wa England na Tottenham anayeuguza jeraha Harry Kane, 26, huenda akarejea katika mazoezi mepesi katika kipindi cha wiki tisa hivi na kwamba anatarajiwa kuanza kuichezea Tottenham kufikia katikati ya mwezi Aprili.. (Telegraph)

Post a Comment

0 Comments