BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO IJUMAA TAREHE 24-01-2020


Manchester United huenda wakamnunua mshambuliaji wao wa zamani Muargentina Carlos Tevez,35, ambaye kwa sasa anachezea Boca Juniors. (Tuttosport)
Tottenham wamekubali kuiuzia Inter Milan kwa euro milioni 20 (£16.8m) kiungo wao wa kati Christian Eriksen, 27. (Sempreinter.com)
Hata hivyo, Barcelona wanataka kumsaini Eriksen ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Denmark mwezi huu wa Januari. (Sky Sports)
Christian EriksenHaki miliki ya picha
Chelsea wamefufua mazungumzo na Lyon kuhusu usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Moussa Dembele, 23, mwezi huu endapo watamkosa Edinson Cavani, 32 kutoka Paris St-Germain's. (Sun)
Manchester United pia wanamnyatia Cavani ambaye ni mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, yuko tayari kujiunga na Barcelona. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Pierre-Emerick AubameyangHaki miliki ya picha
Manchester United bado inapania kumsajili kiungo wa kati wa Leicester James Maddison, 23. (Star)
Chelsea na Barcelona wanamng'ang'nia beki wa Grasshoppe Mswizi Alan Arigoni, 25. (Blick)
Matumaini ya Manchester United ya kumpata Bruno Fernandes yamegonga mwamba baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia bei ya £68m iliyowekwa na Sporting Lisbon kumuuza kiungo huyo wa kati wa Portugal. (Mail)
Bruno FernandesHaki miliki ya picha
Liverpool wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Real Madrid Isco, 27, japo inadai karibu Yuro milioni 70 (£59m) kumuachilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania. (El Desmarque - in Spanish)
Inter Milan wamekataa ofa ya mkopo kutoka kwa Manchester United kumtaka kiungo wa kati wa Uruguay Matias Vecino, 28. (Sky Sports)
Newcastle wako tayari kutoa ofa ya kumnunua beki wa Tottenham, Muingereza Danny Rose, 29. (Evening Standard)
Danny RoseHaki miliki ya picha
Manchester United wanatafakari uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Paris St-Germain Mfaransa Eric-Junior Dina Ebimbe, 19, ambaye kwa sasa yuko Le Havre kwa mkopo. (RMC Sport)
Leicester wamekataa ofa iliyotolewa na Aston Villa kumsaini kwa mkopo Islam Slimani, 31, hadi mwisho wa msimu huu. The Foxes wanataka mkataba wa kudumu kumuachilia mchezaji huyo wa kimataifa wa Algeria, ambaye kwa sasa yuko Monaco kwa mkopo. (L'Equipe via Star)
Inter Milan wameanza mazungumzo na Napoli kuhusu mpango wa kumsajili mshambuliaji wa Uhispania wa miaka 34 Fernando Llorente, ambao utajumuisha klabu hiyo kuachana na mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 33. (Sky Sports)
Fernando LlorenteHaki miliki ya picha
Tottenham wana imani ya kukamilisha mkataba wa kumsaini mshambuliaji wa Real Sociedad Willian Jose lakaini huenda wakalazimika kuongeza juhudi za kumpata kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Brazil kwa kuimarisha ofa yao. (ESPN)
Kiungo wa kati wa Real Madrid, Dani Ceballos, 23, anapania kusitisha mkataba wake wa mkopo wa msimu mzima na Arsenal kwasababu ya kukosa nafasi ya kucheza ili apate nafasi ya kujumuishwa katika kikosi cha kitaifa cha Uhispania katika michuano ya kombe la Euro mwaka 2020. (Sky Sports)
Dani CeballosHaki miliki ya picha
Newcastle wamefikia mkataba wa kumsajili kiungo wa kati wa Inter Milan Valentino Lazaro kwa mkopo kwa lengo la kumnunua kwa £20m mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria msimu wa joto. (Sky Sports)

Post a Comment

0 Comments