BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 16-01-2020




Haki miliki ya picha

Klabu ya Inter Milan imeafikiana makubaliano binafsi na kiungo wa Denmark Christian Eriksen,27, ili wamsajili moja kwa moja lakini klabu yake ya Tottenham inaitaka Milan kuongeza dau lao mpaka Euro milioni 10.

Tottenham wapo kwenye mazungumzo ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji kutoka Cape Verde Ze Luis, 28, anayechezea klabu ya Porto.
West Ham wanasuka mipango ya kumsajili kwa mkopo kiungo wa Chelsea Ross Barkley 26. Mchezaji huyo alishawahi kuhudumu chini ya kocha mpya wa West Ham David Moyes katika klabu ya Everton.
PSG imeitaka Atletico Madrid kupandisha dau lao la usajili ili kumnasa nyota wa Uruguay Edinson Cavani kutoka Euro mioni 10 mpaka 30. Mshambuliaji huyo anamaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu huu.

Christian Eriksen (kulia) alijiunga na Tottenham mwaka 2013
Haki miliki ya picha

Arsenal wanapanga kutoa pauni milioni sita ili kumnasa beki wa kushoto wa wa PSG Mfaransa Layvin Kurzawa, 27, kabla ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu.
Tottenham na mahasimu wao Arsenal ni miongoni mwa vilabu vitano vya ligi ya Primia ambavyo vinamuwinda beki wa Getafe na timubya taifa ya Togo Djene Dakonam, 28. Tayari klabu ya Monaco ya Ufaransa imeshakataliwa maombi yao ya kumsajili.
Spurs watakutana na ushindani kutoka Sevilla katika mbio zao za kutaka kumsajili mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24.


Haki miliki ya picha

Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Brazil Matheus Fernandes, 21, kutoka klabu ya Palmeiras kwa dau la Euro milioni 7, lakini pia kuna uwezekano wa euro milioni 4 kuongezeka.
Miamba hiyo ya Uhispania pia inafuatilia kwa karibu maendeleo ya kiungo kinda wa Japani Jun Nishikawa, 17, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Cerezo Osaka.
Beki wa kushoto Mholanzi Mike van Beijnen, 20, ameondoka Barcelona bila hata kucheza mchezo mmoja miezi sita baada ya kusaini mkataba ambao uliweka sharti la kuuzwa kwa Euro milioni 100.
Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas amedokeza kuwa huenda akaondoka katika klabu ya Marseille baada ya Afisa Mkuu wa zamani wa West Ham na Sheffield Wednesday Paul Aldridge kuteuliwa kuwa 'mshauri maalum' wa klabu bila yeye kufahamishwa

Post a Comment

0 Comments