BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMISI TAREHE 09/01/2020

Arsenal na Manchester United wamewasilisha ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32. (El Chiringuito - via Metro)

Chelsea sasa wanamlenga mlinzi wa West Ham Issa Diop na wanatazamiwa kutuma dau la usajili la pauni milioni 40 kwa Mfaransa huyo mwenye miaka 22. (Express)
Manchester United wanaaminika kutaka kumsajili beki wa klabu ya Hellas Verona ya Italia na raia wa Albania Marash Kumbulla, 19. (Star)
Tottenham, Arsenal na Manchester United wanapigana vikumbo kutaka kumsajili beki wa kati Samuel Umtiti, 26, na klabu ya Barcelona inaonekana imedhamiria kumsajili Mfaransa huyo. (El Desmarque - in Spanish)
De LigtHaki miliki ya picha
Ajax wanapanga kumrudisha beki Matthijs de Ligt, 20, kwa mkopo licha ya kumuuza mchezaji huyo licha ya kumuuza Juventus mwishoni mwa msimu uliopita. (A Bola - in Portuguese)
Chelsea inaonekana haipo tayari kumsajili mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, huku meneja Frank Lampard akiona mchezaji huyo haendani na kikosi chake. (90min)
Crystal Palace wamekataa kumuuza Zaha kwa vigogo wa Ujerumani Bayern Munich. (Guardian)
Wilfred Zaha
Tottenham wamejiunga kwenye mbio za kutaka kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Poland Krzysztof Piatek, 24, huku Milan wakitaka dau la pauni milioni 30. (Guardian)
Spurs hawana mpango wa kutafuta mbadala wa haraka wa kiungo Moussa Sissoko, 30, ambaye ni majeruhi na hatarajiwi kurudi dimbani mpaka Aprili. Hata hivyo, watalazimika kununua kiungo mwengine endapo watawauza Victor Wanyama, 28, na Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)
Everton wanataka kumsajili kiungo wa Juventus, Mfaransa Adrien Rabiot, 24, kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. (Corriere Dello Sport, via Sport Witness)
Arsenal haitarajiwi kufanya usajili wa moja kwa moja mwezi Januari na badala yake watajikita kwenye mikopo. (Goal)

Post a Comment

0 Comments