Chelsea imetoa ofa ya kumsajili mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani, 32, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Times)
Babake Cavani amesema nyota huyo atajiunga na Atletico Madrid ikiwa klabu hiyo ya Uhispania itaafikiana na PSG. (Guardian)
Tottenham wanamlenga mshambuliaji wa Real Sociedad, Mbrazil Willian Jose na kiungo huyo wa miaka 28-anatarajiwa kusafiri London kwa mazungumzo. (AS)
Klabu sita za ligi ya premia zinataka kumsaini beki wa Tottenham Muingereza Danny Rose, 29, mwezi huu. (Sky Sports)
Tottenham wanapanga kutoa ofa ya pili ya kumnunua mshambuliaji wa Fenerbahce na Kosovo Vedat Muriqi. (Aksam, via Sport Witness)
Beki wa Shakhtar Donetsk na Ukrain Mykola Matviyenko, 23, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kuenda Manchester City, yuko katika mazungumzo na Arsenal, ajenti wake anasema. (Football.London)
West Ham imeonesha nia ya kutaka kununua winga wa kimataifa wa Ukochi na Bournemouth Ryan Fraser, 25, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu wa joto. Kiungo huyo pia ananyatiwa na Arsenal na Liverpool. (Mirror)
Everton bado wanamtaka mshambuliaji wa Gremio Mbrazil Everton Soares, 23. (UOL, via Star)
Barcelona wanajitahidi kukamilisha mkataba wa kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Valencia na Uhispania Rodrigo Moreno, 28, baada ya kumkosa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (Sport)
Chelsea wanatafakari uwezekano wa kumuuza kipa wa Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, msimu wa joto, na huenda wakamnunua kipa wa Burnley Nick Pope, 27. (90Min)
Winga wa Uholanzi Tahith Chong, 20, yuko tayari kuondoka Manchester United mwisho wa msimu huu. (Goal.com)
Middlesbrough, Stoke na Derby wanasubiri kuona ikiwa Bournemouth itamruhusu beki Muingereza Jack Simpson, 23,kuondoka kwa mkopo. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Barcelona Quique Setien anasema kuwa klabu hiyo inamtafuta mchezaji atakayeziba pengo lililoachwa na mshambuliaji wa Uruguay aliyeumia Luis Suarez, 32 mwezi huu. (Sport)
Barca inapania kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Rodrigo Moreno lakini Valencia inataka kumnunua kiungo huyo kwa euro milioni 60. (Marca)
1 Comments
Chelsea must sign a perfect striker,or use oliver giroud,because he is able to compete with defenders than Abraham,and also he have experience enough
ReplyDelete