BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO ALHAMIS TAREHE 02 -01-2020

Napoli na Ajax ziko tayari kumpigania Jan Vertonghen, 32, na kuishawishi Tottenham kumuuza beki huyo raia wa Ubelgiji kabla ya kuruhusiwa kuondoka kwa uhamisho wa bure msimu wa joto. (Telegraph)
Marseille na Aston Villa ni miongoni mwa klabu zinazomfuatilia mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge, 30, ambaye kwa sasa anachezea klabu ya Uturuki ya Trabzonspor. (Mail)
Real Madrid imewasiliana na wawakilishi wa mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 27. (Le10Sport)
Sadio ManeHaki miliki ya picha
Manchester United na Tottenham wanatarajiwa kukabiliwa kwa ushindani mkali wa kumnunua kiungo wa kati wa Lille Mfaransa Boubakary Soumare,20, huku ofa sita za kumnunua zikiripotiwa kupokelewa na klabu yake. (Mail)
Kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 27, atalazimika kusubiri mkufunzi wa Arsena Mikel Arteta kutafakari pendekezo lake la kuhamia Hertha, Berlin kwa mkopo mwezi huu wa Januari. (Independent)
Granit XhakaHaki miliki ya picha
Kocha wa Chelsea Frank Lampard amepuuzilia mbali tetesi kuwa anapania kumnunua mshambuliaji wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 27. (Star)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amedokeza kuwa kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, huenda akaondoka katika klabu hiyo pindi mkataba wake utakapomalizika mwisho wa msimu huu. (Mirror)
Jurgen KloppHaki miliki ya picha
Everton imekuwa ikimtaka Moise Kean, lakini haina mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo wa Italia wa miaka 19, ajenti wake anasema. (La Repubblica via Star)
Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon na Ureno Bruno Fernandes, 25, ambaye alikuwa akilengwa na Manchester United, amesema anakaribia kujiunga na Tottenham msimu wa joto kuliko klabu nyingine yoyote. (Express)
Bruno FernandesHaki miliki ya picha
Tottenham wanaongoza kinyang'anyiro cha usajili wa beki wa West Brom Nathan Ferguson, 19, ambaye pia nafuatiliwa na Crystal Palace. (Mirror)

Post a Comment

0 Comments