BETI NASI UTAJIRIKE

TETESI ZA SOKA DUNIANI LEO JUMANNE TAREHE 07-01-2020

Brighton, Crystal Palace na Norwich wanataka kumsajili mshambuliaji wa Tanzania Mbwana Samatta, 27, kutoka klabu ya Genk ya Ubelgiji.(Guardian)
Afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Giuseppe Marotta anasema miamba hao wa Serie A hawajawasiliana na Eriksen kuhusu uhamisho wa Januari. (Football.London)
Inter Milan wamewasilisha dau la £20m kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Denmark Christian Eriksen, 27, lakini mkufunzi wa klabu hiyo Antonio Conte angelipendelea kumsajili kiungo huyo wa kati wa Barcelona Arturo Vidal, 32. (Mirror)

Christian EriksenHaki miliki ya picha

Inter pia wanaongoza Aston Villa na Newcastle katika mbio za kumsaka mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, kutoka Chelsea. (Telegraph)
Reds wanajiandaa kumpatia mkataba mpya kiungo wa kati wa Uhispania Pedro Chirivella. (Sky Sports)
Tottenham inatafakari uwezekano wa kumnunua kwa mkopo kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Ufaransa Thomas Lemar, 24. (Independent)

Olivier GiroudHaki miliki ya picha

Manchester City wanamnyatia beki wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 24, ambaye pia anafuatiliwa na Barcelona na Real Madrid. (Mirror)
Everton wameingia katika kinyang'anyiro cha kumsaini beki wa St Etienne Mfaransa Wesley Fofana, 19, ambaye anatakiwa na klabu kadhaa za Ulaya. (Star)
Manchester United wanamtaka mchezaji wa safu ya kati wa Leicester na England James Maddison, 23, lakini wanafahamu fika kuwa ni vigumu kukamilisha mchakato wa uhamisho mubwa mwezi Januari.
(Sky Sports)

James MaddisonHaki miliki ya picha

Mkufunzi wa Newcastle Steve Bruce amesema klabu hiyo haina mpango wa kuwauza wachezaji wake mahiri baada ya Manchester United kumuulizia Sean Longstaff, 22. (Manchester Evening News)
Liverpool wameweka dau la kumnunua kipa wa Uturuki na Trabzonspor, Ugurcan Cakir,23. (Metro)
Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 34, amefanya mazungumzo na klabu ya zamani ya Wayne Rooney DC United inayoshiriki ligi ya ML. (The Athletic - subscription required)

Luka ModricHaki miliki ya picha

Newcastle wanamtaka beki wa kimataifa wa Sampdoria na Gambia Omar Colley, 27. (Tuttomercato via Chronicle Live)
West Ham wanamfuatilia kwa makini kiungo wa kati wa Benfica na Portugal Gedson Fernandes, 20, ambaye anaweza kuachiliwa kwa £102m kulingana na mkataba wake wa sasa. (Football.London)
Juventus haitamuuza wachezji wake wa safu ya kati Emre Can, 25, ama Adrien Rabiot, 24, mwezi huu wa Januari, amesema mkurugenzi Fabio Paratici, licha ya Manchester United na Everton kuwataka wachezaji hao. (Mail)

Emre CanHaki miliki ya picha

Burnley wanatafakari uwezekano wa kumnunua beki wa kati Scotland na Aberdeen Scott McKenna, 23. (Mail)
Everton wamekuwa wakimfuatilia Fernandes lakini wata mnunua mshambuliaji wa Senegal Oumar Niasse, 29, beki wa Curacao, Cuco Martina, 30 na mshambuliaji wa Uturuki Cenk Tosun, 28, ikiwa hali ya fedha itawaruhusu. (Express)

Post a Comment

0 Comments