BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AWAPIGA MKWALA ALLIANCE FC NA MASHABIKI WAKE WA MKOPO

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc ambao utapigwa leo  Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba


Akizungumza na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Vandenbroeck amesema baada ya mazoezi ya siku mbili, vijana wake wako tayari kuikabili Alliance Fc katika mchezo ambao kama wataibuka na ushindi watajichimbia kileleni kwa kufikisha alama 41

"Tumefanya maandalizi kwa siku mbili baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc. Nimeridhishwa na mwenendo wa wachezaji, wote wako kwenye hali nzuri kuelekea mchezo wa kesho," amesema

Simba imeshinda michezo yote minne iliyopita dhidi ya Alliance Fc.Mabingwa hao wa nchi wanapewa nafasi ya kuendeleza ubabe wao dhidi ya vijana hao wa Alliance Fc

Post a Comment

0 Comments