BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN AELEZEA JINSI ATAKAVYOICHAKAZA MWADUI FC

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vanderboeck ametamba kwamba atawashushia kipigo wapinzani wake Mwadui FC ambao anacheza nao leo Jumamosi kwa kuwa tayari ameshalijua soka la Bongo.


Kocha huyo ametamba kuwa atawashushia kipigo Mwadui FC ambao wanacheza nao kwenye Kombe la Shirikisho (FA) kwa sababu ametambua timu nyingi za hapa nchini zinatumia mfumo wa mipira mirefu.

Kocha huyo amesema kwamba ameshajua mbinu hiyo ya wapinzani wake, ndiyo maana kwa sasa anapata ushindi katika mechi zake zote za ligi na michuano hiyo mingine.

“Kwa sasa nimekaa hapa Bongo nimeshatambua kwamba timu nyingi zinacheza kwa kutumia mfumo mmoja, wanatumia mipira mirefu na karibu wote wanalingana kwa kutumia staili hiyo. 

“Nimeshatambua kwa sasa ndiyo maana unaona tunapata ushindi katika mechi zetu, kwa sababu ninapanga watu ambao wana uwezo wa kukimbia pale ambapo wanapocheza hivyo.

“Tulipata ushindi kwenye mechi zetu zilizopita kule Mwanza na hiyo inatupa nguvu ya kufanya vizuri katika mechi zetu zote ambazo zinakuja,” asema Mbelgiji huyo.

Post a Comment

0 Comments