BETI NASI UTAJIRIKE

MAMBO YA UJANJA UJANJA YAPIGWA CHINI SIMBA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai atazindua kadi za kiektroniki za mashabiki Januari 29, 2020 Bungeni jijini DodomaAkizungumza na waandishi wa habari mapema jana.


Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema, gharama ya kadi hiyo ni shilingi za Tanzania 22,000.Aidha sehemu ya fedha hizo ambazo ni Tsh 14,500 itaingia moja kwa moja kwenye mfuko wa klabu ya Simba

Manara amesema baada ya Spika Ndugai kuzindua kadi hizo nae atakabidhiwa ya kwake kwakua ni mshabiki na mwanachama wa Simba pamoja na wabunge ambao wanawapenda mabingwa wa nchi.

"Januari 29 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai atazindua kadi zetu za mashabiki bungeni.
"Lengo letu tunataka ndani ya mwaka huu tuwe tumeuza kadi laki moja kwa mashabiki," alisema Manara.

Post a Comment

0 Comments