Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amesema sio kweli Simba itapata mgao wa asilimia 20 ikiwa Klabu ya KRC Genk itamuuza mshambuliaji Mbwana Samatta kwenda Aston Villa.
Senzo amedai kuwa mkataba huo wa kupata mgao wa asilimia 20 uliishia pale TP Mazembe ilipomuuza kwenda KRC Genk kwa Sasa Kama Kuna mgao wa kupewa labda TP Mazembe watapewa na Genk na sio Simba.
Hiyo imekuja baada ya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Aden Rage kusema yeye ndio alimuuza Samatta Tp Mazembe na kuweka kipengele Cha Klabu ya Simba kupata mgao wa Asilimia 20 popote pale mshambuliaji huyo atakapouzwa.
Na kaenda mbali zaidi na kuwaambia iwapo viongozi wa Simba walikichezea kipengele hicho kitawatokea puani.
Pia aliyewahi kuwa Kaimu rais wa Klabu ya Simba Salim Abdalah amesema yeye anachojua wanaidai TP Mazembe €50,000 (Zaid ya milioni 120 za Kitanzania) kwa madai ya kwamba kwenye mkataba walikuwa wamekubaliana Simba watapewa mgao wa asilimia 20.
0 Comments