Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, jioni ya leo kinashuka kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikabili Mbao Fc ukiwa ni mchezo wa ligi kuu
Baada ya kupoteza mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi kwa kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar, hii ni nafasi kwa Simba kurejesha furaha ya mashabiki wake
Lakini ni mchezo ambao kocha Sven Vandenbroeck na msaidizi wake Selemani Matola wanapaswa kuwa makini hasa katika uchaguzi wa kikosi kinachopaswa kucheza leo
Kwani tangu wakabidhiwe majukumu ya kuinoa Simba, wamekuwa wakibadili timu karibu kila mchezo
Mbao Fc imekuwa na kawaida ya kutoa upinzani mkali kwa Simba hasa inapocheza kwenye uwanja wake wa CCM Kirumba
Msimu uliopita Simba iliacha alama zote tatu dhidi ya Mbao kwenye uwanja huo
Ushindi kwa Simba utaendelea kuwakita kileleni mwa msimamo wa ligi huku wakizidi kuwaacha mbali watani zao Yanga amao jana walichezea kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Kagera Sugar
0 Comments