BETI NASI UTAJIRIKE

SAMATA ATOA MBINU ZA KUWEZA KUCHEZA ULAYA

Mchezaji mpya wa Astonvilla ya Uingereza Mbwana Ally Samata amewahamasisha na kuwataka vijana wa kitanzania kupambana zaidi ili kufikia malengo yao mbalimbali . Samata ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania kusajiliwa na kucheza ligi kuu Uingereza . Hivi karibuni nyota huyo alifanya mahojiano na kituo cha taelevisheni Ulaya na kutoa hisia zake kwa wapambanaji wote wanaoamini kupitia soka. Samata alinukuliwa akisema 

"Nitakuwa naongopa nikisema sijafanikiwa kwenye maisha lakini pia nina mtazamo tofauti kuhusu maisha kutoka kule nilipokuwa, bado nina ndoto kubwa, hii ni Genk, sio Barcelona au Madrid.

Lengo kubwa ni kucheza kwenye vilabu vikubwa zaidi duniani, vilabu tunavyovipenda, vyenye historia kwenye soka la Ulaya.

Hadi kufanikiwa Afrika nilipewa hamasa, nilitaka kujituma nifike juu kabla ya kuwahimiza Watanzania wenzangu.

Ukiangalia posts zangu za Instagram nataka kuwashauri vijana kuhusu maisha na namna ya kufanikiwa.

Najaribu kutuma ujumbe kwamba kwenye maisha unaweza kuvuka changamoto nyingi lakini mwisho wa siku utafanikiwa tu kama una malengo na kuyafanyia kazi.

Si Watanzania wengi nikiwemo mimi tumezaliwa kwenye familia tajiri, nimehangaika pia, sikuzaliwa hapa Ulaya. Ilibidi niweke jithada kubwa kufika nilipo leo.

Ni rahisi leo mimi kuwaeleza wacheza soka Watanzania kwamba inawezekana kucheza Ulaya kwa sababu nimefanya hivyo tofauti na kama ningewaeleza hivyo wakati bado nacheza ligi za Tanzania.- Mbwana Samatta.

Post a Comment

0 Comments