BETI NASI UTAJIRIKE

SABABU ZILIZOMUONDOA KAMBINI TSHISHIMBI ZAELEZWA

Inaelezwa kuwa kuwa kiungo wa Yanga, Mkongomani, Papy Tshishimbi ametimkia  kwao Congo kuangalia familia yake.Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji, Luc Eymael, alisema Papy alimuaga siku moja kabla ya kuanza nao mazoezi, kuwa anamatatizo ya kifamilia 


hivyo  anasafiri kwenda kuwaona jamaa zake.Hata hivyo alisema amempa siku chache kwa kuwa hajawahi kuwa pamoja nae mazoezini tangu ameanza, hivyo anatakiwa kuwahi ili apate muda wa kumsoma vizuri.

Nimefuatilia baadhi ya video za Yanga, Papy ni mchezaji mzuri, lakini nahitaji awahi kurudi ili afanye mazoezi na wenzake kwani  tuna kazi kubwa  ambayo inatukabili mbele yetu,”alisema Eymael.

Taarifa inasema kuwa, hata hivyo Tshishimbi ameeleza kuwa familia yake kwa sasa ipo salama, hivyo anatarajia kurudi kabbla ya mchezo wao dhidi ya Azam FC.

Sikupanga kuja nyumbani kwa  kipindi hiki lakini imenilazimu kutokana na sababu ambazo zipo nje ya uwezo wangu, lakini nitarudi haraka  sitaki kukosa mechi ya Azam, pia sijahudhuria mazoezi na kocha wetu mpya tangu ameanza,”alisema Tshishimbi.

Post a Comment

0 Comments