BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA:KUNA DE LA BOSS MMOJA TU DUNIANI NAYE NI HAJI SUNDAY MANARA

Saa 4 usiku wa Jumamosi ya January 18, Katikati ya jiji la Dar, Bint mrembo na mng'avu,mtoto wa Mzee Hassan Haji aitwae Bi Rahma anajifungua mtoto mzuri na mwenye afya.



Nakuzungumzia wewe Haji Sunday Ramadhan Manara "De la Boss" mtoto wa nyota wa kwanza Tanzania aliyeanza kucheza soka Ulaya na Asia katika vilabu vya Heracles, New York Eagles, Australian Club na Al Nasri. *Happy Birthday to you Soldier!!!* Tabia ya udadisi,usikilizaji hoja na kupenda kujudge mambo vimekuwa sehemu tu ya kichocheo cha mafanikio yako.

Yes!!, umeweza kuongeza mtaji wa rasilimali watu toka pale kaka Steven Ally alipoutangazia umma wa wana Simba na wanamichezo kwa ujumla kuwa utachukua nafasi ya Kaka Humphrey Nyansio.

Hapo kabla Simba haikuizidi Yanga kwa mashabiki lakini leo wazi kabisa na hili nakiri mie kama mzoefu wa soka hapa nchini,wazi kabisa Simba ina washabiki wengi ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa sehemu ya maendeleo makubwa ya klabu.Pamoja na hayo umefanya hamasa kurejea upya vinapokutana vilabu hivi viwili vya watani wa jadi (Traditional rivals). Wana Simba hatuwezi kusahau slogan kama "This is Simba" ,"Yes We Can" ,"Do or Die" nk

Naandika haya kama mdau mzoefu wa mpira, haijawahi kutokea hapa Tanzania haswa kwa klabu yetu akatokea mtu tena wa kawaida asiye na kipato kuweza kuhamasisha watu kwa namna hii.

Mwenyezi Mungu amwondoshe na adhabu ya kaburi wajina wako aliyekutabiria mema ya kuwa siku moja utakuwa mwenye jina kubwa na jasiri hapa Tanzania.
Wasiofahamu ni kuwa Mzee Hassan Haji (babu yako ) ni miongoni mwa wenyeviti waliowahi kuitumikia klabu yetu ya Simba miaka ya nyuma.

Makala hii imeandikwa na Al Hassan Mbilili, Mwanachama wa klabu ya Simba

Post a Comment

0 Comments