BETI NASI UTAJIRIKE

RONALDO AWEKA REKODI NYINGINE SERIE A

Magoli mawili aliyofunga Ronaldo dhidi ya Parma na kuisaidia Juventus kuibuka na ushini wa mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi kuu Italy maarufu kama Serie A yalimfanya nyota huyo kuweka rekodi nyingine duniani. Mchezaji huyo mwenye miaka 234 alianza kwa kupachika bao la kuongoza dakika ya 43 kwenye dimba la Allianz Stadium kabla ya kufunga bao la pili kipindi cha pili dakika ya 58 

Kwa mara nyingine Ronaldo ameudhihirishia ulimwengu wa soka kuwa bado yuko vizuri baada ya kufunga mechi 7 mfululizo akivunja rekodi ya mchezaji mwenzake wa Juventus David Trezeguet aliyoiweka Disemba mwaka 2005 

Mchezaji huyo mpaka sasa ameshafunga mabao 16 kwenye Serie A katika michezo 20 waliyocheza huku Immobile akiwa nafasi ya kwanza ufungaji akiwa na mabao 23 kwenye michezo 19 aliyocheza.

Mchezaji huyo ameisaidia Juventus kubaki kileleni kwa kufikisha pointi 51 mbele ya Intermilan wanaoshikilia nafasi ya pili kwa pointi 47 wakicheza michezo sawa na Juventus.

Post a Comment

0 Comments