KMC imefanikiwa kwenda Hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 5-0 dhidi ya Pan Africans leo Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC leo yamefungwa na James Msuva dakika ya 12, Serge Tapei dakika ya 22, Sadallah Lipangile mawili dakika za 45 na 73 na Charles Ilanfya dakika ya 78.
Mechi nyingine ya Hatua ya 32 Bora leo, Panama imeibuka na ushindi wa penalti 3-0 dhidi ya Mtwivila City baada ya sare ya bao 1-1 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, KMC na Panama zinaungana na Mbeya City iliyotoa Polisi Tanzania kwa penalti 3-1 baada ya sare ya 1-1 Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro juzi kuingia raundi ya tano.
Hatua ya 32 Bora itaendelea kesho kwa vigogo, Simba SC kumenyana na Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Uhuru.Mechi nyingine za kesho ni kati ya Gwambina na Ruvu Shooting, Africans Sports na Alliance FC, Ndanda FC na Dodoma FC, Ihefu FC na Gipco FC, Mtibwa Sugar na Sahare All Stars, JKT Tanzania na Tukuyu Stars na Kagera Sugar dhidi ya Mighty Elephant.
Jumapili Maji Maji itamenyana na Stand United, Namungo FC na Biashara United, Yanga na Tanzania Prisons na Lipuli na Kitayosa FC, wakati Jumatatu Azam FC itamenyana na Africans Lyon kukamilisha hatua hiyo.
0 Comments