BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: MBEYA CITY YAANZA KUONYESHA UBABE CHINI YA KOCHA MPYA

Mbeya City imefanikiwa kufungua mlango wa hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa penalty 3-1 baada ya sare ya 1-1 



 Polisi Tanzania jioni ya leo Uwanja wa Ushirika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mshambuliaji Mohamed Mkopi alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 42, kabla ya Mbeya City inayofundishwa na Amri Saidi ‘Stam’ kusawazisha kupitia kwa Rehani Kibingu dakika ya 52.


Katika mikwaju ya penalti, Sixtus Sabilo pekee aliifungia Polisi wakati Marcel Kaheza, Hassan Maulid na Shaaban Stambuli walikosa huku penalti za Mbeya City zikifungwa na Rolland Msonjo, Ibrahimu Nduguli na Rehani Kibingu. 


Hatua ya 32 Bora ASFC taendelea Ijumaa kwa mechi mbili zote zikipigwa Jijini Dar es Salaam, Uwanja wa Karume Panama FC na Mtwivila City na Uwanja wa Uhuru KMC dhidi ya Pan Africans.

Jumamosi; Gwambina v Ruvu Shooting, Africans Sports v Alliance FC, Ndanda FC v Dodoma FC, Ihefu FC v Gipco FC, Mtibwa Sugar v Sahare All Stars, JKT Tanzania v Tukuyu Stars, Simba SC v Mwadui FC na Kagera Sugar dhidi ya Mighty Elephant.

Jumapili Maji Maji itamenyana na Stand United, Namungo FC na Biashara United, Yanga na Tanzania Prisons na Lipuli na Kitayosa FC, wakati Jumapili Azam FC itamenyana na Africans Lyon kukamilisha hatua hiyo.

Post a Comment

0 Comments