BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI YA MECHI: HIVI NDIVYO SIMBA ILIVYOICHAKAZA ALLIANCE FC BAO 4-1

Simba SC wamezidi kutanua uongozi wao katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji, Mbao FC jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. 



Kwa ushindi huo, Simba SC inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Sven Ludwig Vandenbroeck imefikisha pointi 41 katika mchezo wa 16, ikiizidi pointi tisa Azam FC inayofuatia katika nafasi ya pili kwa pointi zake 32 za mechi 15.
Katika mchezo huo uliochezeshwa ma refa Martin Saanya wa Morogoro aliyesaidiwa na washika vibendera Jesse Erasmo wa Morogoro na Edgar Lyombo wa Kagera, hadi mapumziko timu hizo zilikuwa zimefungana 1-1.

Alliance FC walikuwa wa kwanza kupata bao, mfungaji Nahodha wake, Israel Patrick Mwenda aliywfunga kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20 baada ya mshambuliaji David Richard kuangushwa na Erasto Nyoni wa Simba. 

Kiungo Jonas Gerald Mkude akaisawazishia Simba SC dakika ya 45 na ushei kwa shuti la umbali wa mita 19 akimalizia pasi ya kiungo wa kimataifa wa Sudan, Sharaf Eldin Shiboub aliyewapiga chenga za kitaalamu mabeki wa Alliance nje kidogo tu ya boksi. 

Kipindi cha pili Simba SC ilirejea na moto zaidi na kufanikiwa kupata mabao matatu zadi, biashara nzuri ikianzishwa na mshambuliaji Mnyarwanda Meddie Kagere aliyefunga bao la pili dakika ya 59 kwa kichwa mpira uliopigwa kwa kichwa pia na beki Muivory Coast, Pascal Wawa kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo Mzambia, Clatous Chama. 

Chama akafunga mwenyewe kwa shuti la mpira wa adhabu kutoka umbali wa mita 20 baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na beki, Geoffrey Luseke dakika ya 63 kabla ya kungo mwingine, Hassan Dilunga kufunga bao la nne dakika ya 77 akimalizia pasi ya Shiboub. 

Kikosi cha Alliance FC kilikuwa; John Mwanda, Israel Mwenda, Mackenzie Ramadhan, Geofrey Luseke, Erick Mrilo, Shaaban William, Martin Kiggi, Juma Nyangi, Michael Chinedu/Shija Mkina dk46, David Richard/Ally Lucha dk87 na Siraj Juma/Sameer Vincent dk67. 

Simba SC; Beno Kakolanya, Shomari Kapombe, Mohammed Hussen ‘Tshabalala’, Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Clatous Chama/Ibrahim Ajibu dk80, Sharaf Shiboub/Gerson Fraga dk77, Meddie Kagere, Hassan Dilunga/John Bocco dk83 na Francis Kahata.

Post a Comment

0 Comments