BETI NASI UTAJIRIKE

RIPOTI KAMILI: MECHI ZA MTIBWA SUGAR , AZAM FC MICHUANO YA MAPINDUZI CUP

Michuano ya Kombe la mapinduzi ilianza rasmi hapo jana kwa michezo miwili. Mchezo wa kwanza ni ule wa Mtibwa Sugar dhidi ya Chipukizi.Mchezo huo ulikuwa ni wa kuvutia pande zote mbili huku haruna Chanongo akiwa mchezaji bora kwa kipindi cha dakika 90.


Kipa Said Mohammed 'Ndunda' akipongezwa na mlinda mlango mwenzake, Abutwalib Msheri baada ya kuokoa penalti mbili na kuiwezesha Mtibwa Sugar kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Chipukizi FC baada ya sare ya 1-1Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kwenye mchezo wa Kund B. 

Chipukizi ilitangulia kwa bao la Suleiman Nassor dakika ya tano, kala ya Haroun Chanongo kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 63.

Nduda aliokoa penalti za Jumaa Kassim na Abdallah Mohamed, wakati mikwaju ya Salim Abui na Abdalla Khalisan ilimpita huku penalti za Mtibwa Sugar zilifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job.



Mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa akishangilia baada ya kuifungia timu hiyo bao pekee dakika ya 57 ikiwalaza Mlandege SC 1-0 katika mchezo wa Kundi A Kombe la Mapinduzi  Uwanja wa Amaan, Zanzibar.                                       

Post a Comment

0 Comments