BETI NASI UTAJIRIKE

REAL MADRID YAENDELEA KUTOA VIPIGO VIKALI LA LIGA

Klabu ya Real Madrid inazidi kuonyesha nia yake ya kutwaa kombe la ligi kuu nchini Uhispania maarufu kama La Liga. Wikiendi hii klabu hiyo ilikaribishwa nyumbani kwa Getafe na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa  mabao 3-0 .


Ushindi huo umeifanya klabu hiyo kuendeleza mbio za ubingwa ikifikisha pointi 40 kwenye michezo 19 iliyocheza sawa na mpinzani wake Barcelona na sasa wametofautiana kwa idadi ya mabao 3 tu huku wote wakiwa na pointi 40

Mabao ya Real Madrid yaliwekwa kimiani na Rafael Varane dakika ya 34 na 53 huku Lukas Modric akifunga bao la tatu dakika ya 90.

Real Madrid imekuwa na msimu mzuri kwa kufungwa mechi 1 tu kati ya 19 ilizocheza huku mshambuliaji wake Karim Benzema akiwa kwenye kiwango cha hali ya juu baada ya kufunga mabao 12 akiachwa nyuma kwa bao moja tu na mchezaji bora wa dunia mwaka 2019 Lionel Messi.

Kuelekea raundi ya pili ya michuano hiyo Real Madrid itaikaribisha Sevilla kwenye mchezo wake wa ishirini utakaopigwa tarehe 18 Januari 2020 huku Barcelona ikicheza na Granada tarehe 19 Januari

Post a Comment

0 Comments