Klabu ya Simba imeendelea na mazoezi makali kujiandaa na mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Alliance FC ya jijini Mwanza. Mchezo huo utapigwa dimba la CCM kirumba
siku ya Jumapili huku Simba wakionekana kutaka kuondoka na pointi zote 6 walizozifuat kanda ya ziwa baada ya kukusanya 3 kutoka kwa Mbao FC mhezo uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 2-1 . Mabingwa hao watetezi wanaongoza lmsimamo wa ligi kuu kwa pointi 38 baada ya kucheza michezo 15. Kwa upande wa Alliance wao wako nafasi ya 13 wakiwa na pointi 20 baada ya kucheza michezo 16. Hizi hapa ni picha za wachezaji wa Simba wakijiandaa na mchezo huo.
0 Comments