BETI NASI UTAJIRIKE

NKWABI NA KILOMONI WALISHAONA JANJA ZA MO DEWJI NDANI YA SIMBA

Mohammed Dewji ameachia ngazi kama mwenyekiti wa bodi ya wakuugenzi ndani ya Simba . Binafsi sijashtua ila ni suala tu la muda lililokuwa linahitajika kujua ukweli wa mambo. Mohammed Dewji aliingia ndani ya Simba kama mwekezaji lakini baadaye alikabidhiwa uongozi wa kuiongoza bodi ya uwekezaji ndani ya Simba. Moja ya wazee wa Simba Kilomoni alikuwa mstari wa Mbele kulipinga suala la Mohammed Dewji kutua klabuni hapo kama mwekezaji na wengi tulimtuhumu kama ni mhujumu wa timu .

Baadaye tulishuhudia aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Swedi Nkwabi akiondolewa nafasi ya uenyekiti wa klabu hiyo kwa madai ya kwamba anaihujumu Simba. Nkwabi alishawahi kuhoji Bilioni  20 za Mohammed Dewji alizonunulia hisa asilimia 49 Simba ziko wapi ?

Ninachokiona kwa Mohammed Dewji ndani ya Simba 

Nyote mnaweza kusema Dewji ni mwekezaji wa Simba ila binafsi naona si mwekezaji bali ni mfanyabiashara ndani ya Simba yaani anaitumia Simba kutangaza biashara zake na hilo linaonekana kwa sasa. Haya ndiyo Mohammed Dewji anayafanya kwa Simba.

1. Kutangaza biashara zake kupitia Simba 

Leo hii Jezi ya Simba imedhaminiwa na kampuni tatu kati ya hizo mbili zinamilikiwa na Mohammed Dewji, swali la kujiuliza ni je Simba wananufaika vipi na matangazo yanayowekwa na mohammed dewji ? Je analipia matangazo hayo ama ni sehemu ya uwekezaji wake ndani ya Simba? . Kama analipia basi anatakiwa aondoe kauli yake ya kusema anatumia zaidi ya biloni 4 kwa mwaka ili kuiendesha Simba .

Kampuni ya Sport Pesa ilitoa bilioni 4.96 kuidhamini klabu ya Simba kwa kipindi cha miaka 5 je fedha hizo hazihusiani na Simba mpaka yeye aseme amewekeza bilioni 4 peke yake .

2. Kulitangaza jina lake kupitia uwanja wa bunju 

Mwaka 2011 uongozi wa Manchester City uliingia mkataba na shirika la ndege la ETIHAD ili tu uwanja wa City of Manchester uitwe ETIHAD STADIUM kwa kipindi 10 ambapo Etihad walilipa paundi milion 120 kwa kipindi hicho . Swali ni je Simba imelipwa shilingi ngapi na Mohammed Dewji ili iweze kuubadili jina la uwanja wake na kuupa jina la Mo Simba arena?.

3. Bilioni 20 ziko wapi ?

Mo alifanikiwa kupata nafasi ya kuwa mwekezaji ndani ya klabu ya Simba baada ya kuyashinda baadhi ya makampuni yaliyojitokeza kufanya uwekezaji ndani ya klabu hiyo mwaka2018 na kuahidi kutoa kiasi cha Sh.Bil 20.

Simba iliingia katika mfumo mpya wa mabadiliko ya klabu kwa kufanya uchaguzi mkuu Novemba 4, mwaka2018  ambao ndio ulimuweka Mkwabi madarakani na kuwa sehemu ya Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo chini ya mwekezaji Mo Dewji ikiwa na wajumbe 16 nane kutoka upande wa mwekezaji nane upande wa wanachama. 


Kiuhalisia Nkwabi na wajumbe wenzake wa bodi walitakiwa kuzidi idadi ya wajumbe wa mwekezaji kwa kuwa walikuwa na hisa 51 na mwekezaji asilimia 49. Kitendo cha Nkwabi kuwa sawa na Mo Dewji kwenye suala la wajumbe ni dhahiri Simba alihujumiwa na hapo ilipaswa suala hilo kuhojiwa kwa umakini. Tuko mwaka 2020 je Mo Dewji ameshatoa hizo bilioni 20 ama tuendelee kuzingojea 

Hitimisho 

Mzee Kilomoni na Swed Nkwabii walishaona janja za Mohammed Dewji ndiyo maana walipambana naye sana lakini mwisho wa siku waliondolewa kwa hujuma na sauti zao zilifungwa. Ni wakati sasa kwa wanasimba kumtafuta Kilomoni na Nkwabi kujua ukweli  wote kuhusu Dewji.

MO DEWJI SI MWEKEZAJI WA SIMBA BALI NI MFANYABIASHARA NDANI YA SIMBA

Post a Comment

0 Comments