BETI NASI UTAJIRIKE

JANUARY MAKAMBA AWAVAA WADHAMINI WA KLABU ZA SIMBA NA YANGA

Aliyewahi kuwa waziri wa Muungano na Mazingira Bw.January makamba ameyavaa makampuni ya kamali yanayodhamini timu mbalimbali ikiwemo Sportpesa inayodhamini klabu za Simba na Yanga akiitaka kampuni hiyo pamoja na klabu hizo kuondoa baadhi ya vipengele vya udhamini ikiwemo  kuweka matangazo hayo kwenye kurasa rasmi za vilabu hivyo na hata jezi za watoto kutochapishwa zikiwa na mdhamini huyo au makampuni ya kamali Makamba amenukuliwa akisema 

"Narudia. Si sahihi kwa klabu za mpira kutumia mitandao yao rasmi kuhamasisha kamari. Kudhamini Jezi ingetosha. Kama @TZSportPesa wamesisitiza hii iwe kwenye mkataba, basi wanaichukulia Afrika kwa mtazamo tofauti kwasababu kipengele kama hiki hakipo kwenye mkataba wao na Everton.


Vilevile, replica za jezi za watoto hazipaswi kuna na nembo za kampuni za kamari lakini hapa klabu zetu zinatengeneza na kuwafanya watoto watangaziane biashara ya kamari".- Mbunge wa Bumbuli January Makamba.

Post a Comment

0 Comments