BETI NASI UTAJIRIKE

NAHODHA YANGA ATOA SABABU ZA KUFUNGWA NA AZAM FC

Nahodha msaidizi wa Yanga Juma Abdul amesema pamoja na kupoteza michezo miwili mfululizo, watarejesha makali yao.Akizungumza baada ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Azam Fc, Abdul amesema matokeo hayo hawakuyatarajia kwani walikuwa wamejipanga kuibuka na ushindi
"Kama wachezaji tumepambana tangu dakika ya kwanza lakini bahati haikuwa kwetu," amesema

"Tumetengeneza nafasi nyingi lakini hatukuzitumia wenzetu wamepata nafasi moja, wameitumia.Aidha Abdul amewataka mashabiki wa Yanga kutokata tamaa na timu yao kwani kila kitu kitakuwa sawa

"Tunawaomba mashabiki wetu waendelee kutuunga mkono. Lazima wafahamu kuna mabadiliko yametokea kwenye timu yetu. Mwanzo tulikuwa na Zahera, alipoondoka tukawa na Mkwasa kwa muda na sasa tunae kocha mwingine"

"Kila kocha ana mbinu zake ambazo tunahitaji muda kuweza kuzishika. Lakini pia kuna wachezaji wameondoka na wengine wapya kusajiliwa, nao wanahitaji muda kuzoea.Mwalimu bado anatengeneza timu, mashabiki wawe na subira, tutakuwa sawa kama zamani"

Post a Comment

0 Comments