BETI NASI UTAJIRIKE

FIGISU ZA YANGA KUMMALIZA NYOTA WA SIMBA KWA TFF

Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Steven Mguto, amesema beki kisiki wa Simba Pascal Wawa amepelekwa katika kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka (TFF), kutokana na madai ya kumfanyia madhambi ya makusudi mshambuliaji wa Yanga, Ditram Nchimbi.


Wawa inadaiwa kufanya tukio hilo katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliozikutanisha timu za Simba na Yanga Januari 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa video inayosambaa inaonyesha katika mchezo ule Wawa alimkanyanga Nchimbi  jambo ambao si la kiungwana katika soka.
Mguto amsema kwa sababu suala hilo halikuwapo katika ripoti ya mwamuzi wala  kwa kamisaa wa mchezo,  lakini video yake mtandaoni  inazua gumzo.
 “Katika kamati hiyo wataiangalia na kuona kama kilikuwa kitendo cha makusudi au laa,  lakini pia watatushauri kamati ya uendeshaji wa ligi jambo gani la kufanya.

“Hatuionei timu yoyote kwetu Simba, Yanga na timu nyingine zote tunazisimamia kwa usawa hatuwezi kupendelea upande mmoja,”

“Bila shaka suala la madhambi yaliofanywa na Wawa litamalizika hivi karibuni kwa sababu tayari video ya tukio zima tunayo na kuiwasilisha sehemu husika, ” Mguto alinukuliwa 

Post a Comment

0 Comments