BETI NASI UTAJIRIKE

MOLINGA AMTUMIA SALAMU KAGERE KIATU CHA DHAHABU

Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga, David Molinga, amesema kuwa kazi ndiyo kwanza imeanza Yanga, hivyo mashabiki wa timu hiyo wasiwe na hofu mambo mazuri yanakuja.


Molinga ametoa kauli hiyo baada ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United ambayo juzi Jumatano ilichezwa kwenye Uwanja wa Namfua na kumalizika kwa Yanga kushinda mabao 3-1, huku Molinga akiifungia moja kati ya hayo.

Molinga alisema kuwa mambo mazuri yanakuja Yanga hivyo wapenzi na mashabiki wa timu hiyo hawatakiwi kukata tamaa. Alisema hapo mwanzo kikosi kilikuwa bado hakijaelewana vizuri lakini kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele wanazidi kuwa bora.

Kwa hiyo, kasi hii tuliyoanza nayo dhidi ya Singida ndiyo hiyo tutaendelea nayo katika mechi zetu zote zilizobakia,” alisema Molinga 

ambaye sasa ameshafunga mabao matano katika Ligi Kuu Bara wakati anayeongoza kwa kuzifumania nyavu kwa sasa ni Meddie Kagere wa Simba, yeye ameshafunga mabao 11.

Post a Comment

0 Comments