BETI NASI UTAJIRIKE

MIPANGO YA YANGA MCHEZO NA AZAM FC LEO JIONI

Meneja wa Yanga Abeid Mziba amesema wataingia kivingine kuikabili Azam Fc katika mchezo wa ligi kuu ambao utapigwa leo Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa.



Mziba aliyeteuliwa mwezi uliopita kushika nafasi hiyo iliyoachwa na Dismas Ten, amesema wamejipanga vema kuwakabili Azam FC, makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita yamerekebishwa na leo wanatarajia kupata matokeo mazuri.

Mziba amebainisha kuwa wachezaji wameahidi kupambana kuhakikisha wanarejea katika kasi ya ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kulitwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo linashikiliwa na watani zao Simba.

Meneja huyo aliongeza kila mchezaji anataka kuonyesha bado wanahitaji kutwaa taji hilo hivyo watapambana katika mechi ya leo na nyingine zitakazofuata za ligi hiyo.

"Kila mechi ina changamoto zake, tumeshaweka mambo sawa sawa, tunawakumbusha pia kuongeza umakini na kutumia vizuri nafasi tunazotengeneza, hakuna mechi rahisi katika ligi na ukimruhusu mpinzani wako kukukamata, ni vibaya, tuliona tulipokosea, hatutarudia makosa," amesema

Baada ya kupoteza mchezo uliopita kwa kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, Yanga inahitaji kupata ushindi leo ili kurejesha furaha ya mashabiki wake

Post a Comment

0 Comments