BETI NASI UTAJIRIKE

MCHAMBUZI : SIMBA KUWENI MAKINI DEWJI ANATAKA HISA NYINGINE

Jana usiku mwekezaji wa Simba Mohammed Dewji aliweka ujumbe ulioashilia anamwaga manyanga ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na anabaki kama mwekezaji wa kawaida ndani ya Simba . Kila mwanasimba na asiyekuwa mwanasimba alitoa ya moyoni


 na wengi wao walitumia hisia kuandika na si utafiti yakinifu . Mchambuzi wa masuala ya kijamii,michezo na hata siasa Maggid Mjengwa amekuja na hoja za msingi na nimenukuu kama alivyoandika 

Tafsiri Ya Kilichotokea Jana Usiku:
Mo Ana Akili Sana..
Ilivyo kwenye ‘ siasa za mpira wa Bongo’ Mo Dewji atarudi, lakini kwa masharti.
Ni hapa tutapoona kuwa Simba ni Wapenzi, na wanachama hushinikizwa na wapenzi.
Kwenye soka furaha ya wapenzi wa timu ni mafanikio ya uwanjani. Wapenzi wa Simba wameshaona kupitia msimu uliopita, kuwa timu yao ina uwezo wa kufanya makubwa hata Kimataifa.
Wapenzi wa Simba haraka watataka kujua kinachomkwamisha Mo kwa sasa ndani ya klabu kuweza kufanya makubwa. Kama yapo, na kama Mo atatoa masharti ya kuondolewa kwa yanayomkwamisha ili arudi, basi, kuna hata uwezekano wa kuyaona maandamano ya wapenzi kwenda klabuni kushinikiza mabadiliko.
Kwamba kuna presha kubwa kwa Mo kutoka kwa wapenzi wa Simba itakayokuja.
Naziona ishara za huko baadae Mo kurudi Simba akiwa na asilimia nyingi zaidi za umiliki wa klabu, na hivyo mamlaka zaidi ya kufanya maamuzi ya kuleta mabadiliko ya kimsingi klabuni, ikiwamo mamlaka ya kuchagua timu ya kiufundi ya watakaomsaidia kuipeleka Simba kwenye ‘ Next- Level’.
Na tusubiri kuona.
Maggid

Kwa haraka haraka naweza kusema uchambuzi wa Maggid ni sahihi lakini pia una ukweli ndani yake . bado nasubiri kuona je aliyoyaandika yatatimia 

Post a Comment

0 Comments