BETI NASI UTAJIRIKE

MAZOEZI WANAYOPIGA WACHEZAJI SIMBA YAGEUKA GUMZO MWANZA

Umeshawahi kuona Simba wanavyopiga mazoezi hasa pale wanapokaribia kucheza Mechi? Binafsi nimeshuhudia mara kadhaa pale Loyola enzi hizo hawana uwanja wa mazoezi pale Bunju. Wachezaji wa klabu hiyo hapo jana walifanya mazoezi ya kufa mtu kujiandaa na mchezo dhidi ya Mbao FC utakaopigwa dimba la Kirumba jioni ya leo. www.amospoti.com inakuletea picha mbalimbali za wachezaji wa Simba wakifanya mazoezi yake ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo. Mashabiki wa soka Mwanza wamesema mazoezi hayo ni kama mechi ndogo baina ya wachezaji wa Simba . Hizi hapa picha John Bocco,Clatous Chama na Mohammed Hussein wakifanya mazoezi ya short passes na kutengeneza nafasi unapousubiri mpira Mohammed Hussein akitoa pasi huku akimzuia Francis Kahata asiweze kuupata mpira Fraga akiutuliza mpira na kumzuia Ajib asiweze kuuchukua . Hawa wote ni viungo huku Ajib akicheza kiungo mshambuliaji na Kahata ni kiungo mkabajiSantos ,Bocco na Kapombe wakipasha misuli moto kwenye mazoezi yaliyofanyika uwanja wa CCM kirumba mwanza 


Post a Comment

0 Comments