BETI NASI UTAJIRIKE

MASHABIKI WA YANGA WAJIPANGA KUANDAMANA MPAKA MAKAO MAKUU

Baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara juzi, mashabiki wengi wa Yanga wamefunguka wakiutaka uongozi wa timu hiyo uachane na kocha mpya.


Hasira za kutaka maamuzi hayo yafanyike ni kutokana na kupoteza mechi mbili mfululizo chini ya Luc Eymael.

Kabla ya kupoteza dhidi ya Azam, Yanga ilipoteza pia mechi ya nyuma yake iliyokuwa dhidi ya Kagera Sugar ambayo ilifungwa kwa mabao 3-0.

Kutokana na mwendelezo wa matokeo hayo, wengi wao wamesema ni vema kazi hiyo akaendelea nayo Mkwasa sababu alianza kuirudisha timu katika morali tofauti na Luc ambaye amekuja kuanza upya.

Mbali na kushinikiza kocha huyo aondolewe klabuni hapo baadhi wamesema wataandamana mpaka makao makuu ya klabu hiyo ili kumuondoa kwa nguvu kocha huyo na kama uongozi utambakiza basi ujiandae kung'olewa madarakani kwani unaonekana haujali hisia za mashabiki wa timu hiyo

Post a Comment

0 Comments