Hii hapa rekodi yenyewe
Klabu hiyo yenye maskani yake Carrington ilianza mwaka 2020 kwa kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal ,Mchezo wa pili ikatoka sare ya bila kufungana dhidi ya Wolves kombe la FA na hapo jana imepigwa mabao 3-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Carabao Cup .mchezo huo uliochezwa dimba la Old Trafford na kuhudhuliwa na watu maarufu akiwemo Wayne Rooney,Paul Scholes na Sir Alex Ferguson.
Bao la kwanza kwa upande wa Manchester City lilifungwa na Bernaldo Silva dakika ya 17, Bao la pili lilifungwa na Riyad Mahrez dakika ya 33 na Andres Pereira alijifunga bao dakika ya 38. Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Manchester City ilikuwa mbele kwa mabao 3-0. Dakika ya 70 Rashford aliipa Manchester United bao la kufutia machozi na mchezo kukamilika kwa manchester city kuingia fainali ya Carabao Cup.
0 Comments