BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER UNITED INAVYOHAMIA SERIE A KIMYA KIMYA

Ashley Young amekamilisha dili lake la kujiunga na klabu ya Inter Milan.Beki huyo mwenye miaka 34 hakuwa tayari kubaki ndani ya United ambayo ilikuwa na mpango wa kumuongezea mkataba mpya amejiunga na Inter Milan kwa kandarasi ya miezi sita.

Young alijiunga na United mwaka 2011 kwa sasa amesema kuwa ni muda wake wa kuwa nje ya United kutafuta changamoto mpya.
Young anakuwa ni mchezaji wa tatu kwa msimu huu kuhamia Italy baada ya Apexis Sanchez , Romelu Lukaku kuhamia Inter milan mwanzoni mwa msimu huku pia beki Chris Smalling akitua AS ROMA
Inter Milan inashiriki Serie A nchini Italia ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 19 vinara ni Juventus wana pointi 48 wamecheza mechi 19 huku United timu yake ya zamani kwenye Ligi Kuu England ipo nafasi ya tano na pointi zake 34 baada ya kucheza mechi 22.

Post a Comment

0 Comments