BETI NASI UTAJIRIKE

MANCHESTER CITY HAO RAUNDI YA NNE FA ,MAN UNITED YAPONEA CHUPU CHUPU KWA WOLVES

Michuano ya chama cha soka Uingereza maarufu kwa jina la EMIRATES FA CUP iliendelea hapo jana huku timu imu zilizokuwa zikitazamiwa kuwa kivutio ni Manchester United ikikaribishwa na Wolves na ule wa Manchester City ikiikaribishaPort Vale


Wolves vs Machester United 

Wameendelea kukumbwa na zimwi la kutoshinda baada ya tarehe 1 mwaka huu kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Arsenal. Hapo jana walikuwa na kibarua kigumu kwenye mchezo wa rundi ya tatu dhidi ya timu ngumu ya Wolves na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila kufungana . Manchester United iliwatumia Greenwood,James, T.Chong na Juan Mata kwenye safu ya ushambuliaji lakini haikupata bao lolote.

Manchester City vs Port Vale 

Pep Guardiola ameonekana kuwa na njaa ya vikombe msimu huu baada ya kuingiza kikosi kikali dhidi ya Port Vale. Kwenye mchezo huo Manchester City waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 huku wafungaji wakiwa ni Zinchenko ,Aguero,Taylor na Foden. Goli la kufuta machozi kwa upande wa Port Vale lilifungwa na Tom Pope. Kwa matokeo hayo Manhester City imefuzu kuingia raundi ya 4ya michuano hiyo.

Leicester City vs Wigan Athletic

Leicester City imezidi kuonyesha kiwangi kizuri kwa kushina mbao 2-0 dhidi ya Wigan Athletic. Tom Perce alijifunga dakika ya 19 kabla ya Barnes kupata bao la 2 dakika ya 40 . Kwa matoko hayo Leicester imefuzu raundi ya 4 ya FA.

Matokeo mengine 

Portmouth 2-1 Fleet wood

Norwich 4- 2 Preston

Bournemouth 4-0 Luton Town

Michezo mingine itaendelea hii leo kwa Chelsea vs Notting Forest ,Liverpool va Everton,Tottenham vs MiddlesBrough na Arsenal Vs Leeds.


Post a Comment

0 Comments