BETI NASI UTAJIRIKE

MANARA AWAPA YANGA MBINU ZA KUCHEZA DHIDI YA SIMBA

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amemtaka Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa, kuhakikisha anacheza dhidi yao bila kufunguka.Manara amemtaka Mkwasa 


kuhakikisha anacheza mchezo wa aina hiyo ili kuepukana na kichapo cha mbwa mwizi ambacho Yanga wanaweza kukipata.

Amemtaka acheze kwa kujilinda zaidi ili walau aweze kupunguza idadi ya mabao kama vile ambavyo Kocha wa Ndanda FC, Meja Mstaafu, Jenerali Abdul Mingange ambaye aliweza kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Simba mechi ya mwisho.

"Kama Mkwasa anataka atoke salama katika mechi ya Jumamosi ni vema akacheza mchezo wa kufunguka.

"Hii itasaidia asiweze kufungwa mabao mengi, lakini akicheza bila kujilinda kwakweli ataondoka na aibu".Post a Comment

0 Comments