BETI NASI UTAJIRIKE

MAKALA: JE NI WAKATI SAHIHI KWA ALIKO DANGOTE KUINUNUA ARSENAL?

Tajiri namba moja Afrika, Mnigeria Aliko Dangote anahusishwa tena na taarifa za kutaka kuinunua klabu anayoishabikia ya Arsenal.Tofauti ni kuwa safari hii, duru zinasema kuwa jambo hilo linaweza kutokea mwaka 2021.

Dangote amenukuliwa na shirika la habari la Bloomberg akisema kuwa: 'Ni timu ambayo ndiyo nataka kuinunua, lakini ninachosema ni kuwa (kampuni) yangu ina miradi ya dola bilioni 20 ambayo kwanza inabidi niikamilishe... labda kufikia 2021 tutaweza (kuinunua Arsenal)."
Toka Septemba 2018 bilionea Stan Kroenke ndiye mmiliki pekee wa klabu hiyo.
Haki miliki ya picha
Hata hivyo, mashabiki na baadhi ya wachambuzi wa kandanda wamekuwa wakimtuhumu tajiri huyo ambaye anamiliki vilabu vya michezo mingine kama kikapu nchini Marekani kuwa haweki kipaumbele katika uwekezaji ndani ya Arsenal.
Mashabiki wamekuwa na hamu ya kuona wachezaji wenye majina makubwa wakisajiliwa, jambo ambalo bado halifanyiki.
Japo kuna ambao wanaoamini Dangote anaweza kubadili mambo, lakini hapo kabla aliwahi kuahidi kuinunua klabu hiyo lakini biashara haikufanyika.
Mwaka 2017 alitamba kuwa anatarajia wamiliki wa klabu hiyo wangeondoka mara tu baada ya yeye kuwasilisha ofa yake.
Julai 2018 akaliambia shirika la habari la Reuters kuwa: "Tutainunua Arsenal kuanzia mwaka 2020… hata kama kuna mtu mwingine atainunua, tutaendelea kuifuatilia tu."Kwa mujibu wa jarida la mambo ya fedha na utajiri la Forbes, Dangote ana utajiri wa dola bilioni 10, huku Kroenke akiwa na dola bilioni 9.7.Hivyo Dangote amemzidi mwenzake kwa dola milioni 300 tu.
Kinara wa kifedha katika ligi ya EPL ni mmiliki wa Chelsea bilionea wa Kirusi Roman Abramovich.
Toka tajiri huyo ainunue klabu hiyo mwaka 2003 mafanikio makubwa ikiwemo kunyanyua mataji ya EPL na hata taji la Klabu Bingwa Ulaya.
Mmiliki wa Wolves Guo Guangchang ana utajiri wa dola bilioni 7.2.

Post a Comment

0 Comments