BETI NASI UTAJIRIKE

LIVERPOOL BADO HAISHIKIKI LIGI KUU UINGEREZA

Unaweza kusema msimu huu wa 2019/20 klabu ya Liverpool imeamua kuudhihirishia ulimwengu jinsi ilivyo bora. kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1990 mpaka mwaka 2020 klabu hiyo haikuwahi kushinda mechi 20 mfululizo za ligi kuu Uingereza ila kwa msimu huu 


wameweza kuweka rekodi kwa kucheza michezo 20 wakipata sare moja tu dhidi ya Manchester United huku nyingine 19 wakitoa vipigo vikali.Tumeshuhudia  timu kama Manchester City na Leicester City zikifungwa kwa urahisi na Liverpool.

Hapo jana klabu hiyo ilitoa ilianza raundi ya pili ya Ligi kuu Uingereza kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Shiffield United huku Mohammed Salah akifunga bao dakika ya  4 na Sadio  Mane akifunga bao la pili dakika ya 64. Kwa matokeo hayo Liverpool inazidi kujikita kileleni mw ligi ikiwa na pointi 58 na mchezo mmoja mkononi huku Leicester City ikiwa nafasi ya pili ikiwa na pointi 45,Manchester City nafasi ya 3 ikiwa na pointi 44 huku Chelsea wakiwa nafasi ya 4 kwa pointi 36.

Post a Comment

0 Comments