BETI NASI UTAJIRIKE

LIPULI WAFANYA KUFURU USAJILI WA DIRISHA DOGO

Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga,  Mlinda Mlango, Deogratius MunishI ‘Dida’ ni miongoni mwa wachezaji wapya tisa waliojiunga na Lipuli FC katika kipindi kifupi cha usajili (dirisha dogo) kilichofungwa Januari 15, 2020.


Dida ambaye msimu uliopita alikuwa akiwatumikia mabingwa Tanzania Bara Simba SC kabla ya kutemwa mwanzoni mwa msimu huu, alikuwa hana timu yoyote, hivyo Lipuli imemsajili kama mchezaji huru,  lengo likiwa kuimarisha eneo hilo la ulinzi wa lango lao.

Wengine waliosajiliWA Lipuli ni pamoja na:

Isihaka Luhago – Azam FC.
David Mwantika – Azam FC.
Ally Myovela – Tanzania Prisons.
Peter Mwangosi – Alliance FC (mkopo).
Paul Ngalema – Namungo FC (Mkopo).
Said Musa – Yanga SC (Mkopo).
Joseph Mtamaki – Mchezaji huru.
Shaaban Adda – Mchezaji huru.

Lipuli FC pia imetema wanne katika kipindi hicho ambao ni Rajabu Mpululo, Dereck Karulika, Waziri TajirI na Shaban Kimaro.

Post a Comment

0 Comments