BETI NASI UTAJIRIKE

LEMUTUZ AMCHANA HADHARANI MOHAMMED DEWJI KISA SIMBA

Mwanaharakati na Shabiki wa klabu ya Simba William Malecela maarufu kama Lemutuz amemtaka mwekezaji wa klabu hiyo bwana Mohammed Dewji kuacha Simba iongozwe na 


jopo la wataalamu wa soka huku yeye akikaa pembeni kama mwekezaji wa timu . Lemutuz amefikia hatua ya kuandika ujumbe huo baada ya kuona Mohammed Dewji anaiongoza Simba kimihemko zaidi huku akikiuka kauli za uwekezaji na uongozi wa timu . 

Hivi majuzi kupitia mitandao yake ya kijamii Mohammed Dewji alitangaza kujiondoa nafasi ya Uenyekiti wa bodi ya wakurugenzi baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar wenye fainali za kombe la Mapinduzi. Siku iliyofuata mwekezaji huyo alifuta ujumbe huo na kujisafisha kwa wanasimba huku akibaki kama Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Simba . Suala hilo liliwakera mashabiki wa Simba huku wengi wao wakimtukana Mo dewji na wengine kumtaka aachane na timu hiyo. Kwa upande wa Mfalme wa mitandao ya kijamii "Lemutuz" aliandika hivi kupitia Instagram 

"Wabongo tuna tatizo sana na the meaning of .."DIVISION OF LABOUR" sijui kwanini huwa tunaamini tunaweza kufanya kila kitu wakati ukweli ni kwamba hatuwezi .....WAWEKEZAJI wetu wa Mpira ndio makosa yao namba moja wanataka Kuwekeza na Kusimamia Mpira HAIWEZEKANI mambo ya Mpira yana wenyewe .....Muwekezaji kazi yako inatakiwa kuwa Kuwekeza tu na kukaa pembeni kudai matokeo kutoka kwa Wahusika .....please Wawekezaji huko Yanga na Simba waachieni wahusika wa Mpira kwani tatizo lipo wapi si kuna watu wameajiriwa kwa ajili ya kusimamia mpira katika hizo timu? ....I mean waachieni hao Muwekezaji hatakiwi kuwepo mbele mbele mara sijui kusajili Wachezaji mara kuahamisha Wapenzi wa Timu ninasema HAPANA hii sio kazi ya Muwekezaji ndio maana hizi timu zetu zinafanya vibaya sana WAWEKEZAJI HEBU RUDINI NYUMA waachieni wahusika haya mambo nyie Wekezeni tu subirini matokeo kama ni mabaya si unafukuza watendaji tu ...lakini sio kujiingiza ingiza mambo kila siku ya Timu mnazifelisha hizi timu U know! .....TAKE IT OR LEAVE IT but I just said it U know and ...THIS CASE IS CLOSED! - @lemutuz_superbrand

Post a Comment

0 Comments