BETI NASI UTAJIRIKE

SAFARI YA TAIFA STARS KUCHEZA KOMBE LA DUNIA 2022 YANUKIA HUU NDIO MPANGO MZIMA

Kwa Mara nyingine tena ndani ya Jiji la Cairo nchini Misri majira ya Saa mbili za Usiku hii leo, Droo ya mzunguko wa pili ya kufuzu kwa Fainali za Kombe la Dunia kwa Mataifa ya Afrika itafanyika


Jumla ya Mataifa 14 yaliyofuzu kutoka Raundi ya kwanza, yataungana mataifa mengine ya 26 ya Viwango vya juu katika FIFA Ranking kukamilisha mataifa 40 yatakayoingia katika Droo hii.

Katika Jumla ya mataifa 40 ya Kiafrika yatashiriki katika hatua ya kufuzu ya kwa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2022, lakini ni Nchi tano tu kati ya hizo zote ndio watakaowakilisha bara huko Qatar

Utaratibu ni kama Ifuatavyo;
Washindi 14 wa raundi ya kwanza wanajiunga na timu 26 za Viwango vya juu kwenye Viwango vya Ubora wa Soka Duniani katika mwezi wa Disemba 2019. Timu hizi 40 zitagawanywa katika Makundi 10 ya timu nne.
Katika kila kundi, timu zitacheza kila mmoja nyumbani na Ugenini katika muundo wa ligi ndogo
Vinara wa Makundi yote kumi watafuzu Moja kwa moja Raundi ya tatu na ya mwisho, ambapo zitapangwa kucheza mechi za nyumbani na Ugenini kisha kupatikana washindi watano hao ndio watafuzu Kombe la Dunia huko Qatar 2022.
Kila kundi litatoa timu moja kutoka kwa kila Chungu. Katika kila kundi, timu ya Pot 1 itashika nafasi ya kwanza, timu ya Pot 2 ya pili, na kadhalika.

Vyungu hivyo viko hivi;
Pot 1: Senegal, Tunisia, Nigeria, Algeria, Morocco, Ghana, Misri, Cameroon, Mali, Congo DR.

Pot 2: Burkina Faso, Ivory Coast, Afrika Kusini, Guinea, Uganda, Cape Verde, Gabon, Benin, Zambia, Congo.

Pot 3: Madagascar, Mauritania, Libya, Msumbiji, Kenya, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Zimbabwe, Niger, Namibia, Guinea-Bissau

Pot 4: Malawi, Angola, Togo, Sudan, Rwanda, Tanzania, Guinea ya Ikweta, Ethiopia, Liberia, Djibouti
Kama inavyoonekana hapo juu, Tanzania iko chungu cha nne

Post a Comment

0 Comments