Klabu ya Yanga ilipoteza mchezo wake wa ligi kuu Tanzania Bara kwa kipigo cha mabao 3-0 walichokipata kutoka kwa Mtibwa Sugar. Wengi walitegemea tukio la kufungwa lingeibua vurugu miongoni mwa mashabiki wa timu hiyo lakini mambo yalikuwa ni tofauti
Kwani baada ya wachezaji hao kutoka uwanjani mashabiki wa Yanga walijipanga msitari kutoka mlangoni mpaka lilipopaki basi la wachezaji hao na kuanza kuwapigia makofi wakiwapa moyo kwa michezo mingine inayofuata na walionyesha kuwa na imani na kocha mpya Luc.
Video: Yanga wakitoka uwanjani baada ya kufungwa 3-0 na Kagera Sugar
Kwa upande wa Simba mambo huwa ni tofauti kwani tulishuhudia aliyekuwa mwalimu wa timu hiyo Patrick Aussems na wachezaji walirushiwa chupa na hata kutukanwa hadharani . Tabia hiyo ya mashabiki wa Simba imeendelea kuonekana hata hapo juzi wakati timu hiyo ikiwasili kutoka Zanzibar baada ya kufungwa mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa Sugar mashabiki waliokuwa Bandarini Dar es salaam waliwapokea kwa kuwazomea wachezaji kitu ambacho kiliwavunja moyo.
Video: Simba wakiwasili kutoka Zanzibar baada ya kufungwa 1-0 na Mtibwa sugar
0 Comments