BETI NASI UTAJIRIKE

KUELEKEA DERBY: UJUMBE WA ALLY KAMWE WAMLIZA HAJI MANARA

Mchambuzi kinda wa kituo cha Azam TV anayefahamika kwa jina la Ally Kamwe ameibua hisia kwa mashabiki na wadau wa soka la nyumbani baada ya kuandika ujumbe uliomlenga msemaji wa klabu ya Simba na mhamasishaji wa timu ya taifa Haji Manara. Mchambuzi 


huyo kijana aliandika hivi. HAJI MANARA "Naiwaza siku yake ya mwisho itakavyokua 😞
Kwenye chumba kimoja, katika moja ya nyumba pale Kariakoo, kila kitu kitatolewa nje na pazia zito litawekwa mlangoni
Ni vitu viwili tu vitakavyotakiwa kuingia ndani kwa wakati huo, kitanda cha kamba na mwili wa Haji Manara.
Safari hii, hataingia kwa miguu yake, ataingia kwa kubebwa. Hatavaa tena ile suti yake nyeusi yakupendeza, siku hii atavalishwa mavazi meupe yakuogopesha.
Macho yatafumba. Mdomo wake utanyamaza. Vipande vya pamba vikichomoza kwenye tundu za pua zake. Ni ndugu wachache tu ndio watakaoruhusiwa kuingia kumtazama.
Nje, maelfu ya watu watakua wamejigawa makundi kwa makundi wakizungumza hili na lile kuhusu Haji.
Viongozi wa kisiasa, viongozi wa mpira, Masheikh, Maaskofu, Wasanii, Wachezaji na marafiki wa Haji, aliokua akiwajua na asiowajua, utawaona kwenye mkusanyiko huu
Wote watakua wakiusubiri mwili wake kwa ajili ya kuuswalia na kumsindikiza katika nyumba yake ya milele. Kaburini.
Pengine siku hii ikija ndipo tutakapojua thamani ya Manara kwenye mpira wetu.
Pengine hii ndio siku tutakapokua tayari kutoa sifa za Haji ambazo tunashindwa kuzisema sasa.
Kwanini nasema hivi? Leo, nimemsikiliza kwa makini Haji kwa saa mbili alizotumia ndani ya Studio ya Wasafi FM
Alikua Haji mmoja aliyekua na sura tano tofauti
Kuna wakati alisimama kama msemaji wa Simba, akaisifia sana timu yake.
Ghafla akawa mtani wa Yanga, akawatania sana. Hata mashabiki wa Yanga waliopiga simu 'walienjoy' utani wake.
Dakika chache baadae, akaeleza kitaalamu changamoto za foleni ya kuingia uwanjani.
Akatoka hapo, akaanza kutoa historia ya Simba na Yanga. Akarudi mpaka miaka ya 1980. Mbele kidogo akaeleza ugumu wa 'derby' hii.
.
.
Wapi katika mpira wetu unaweza kumpata mtu wa aina ya Manara?
Tuna wasemaji wengi nchini, lakini bahati mbaya wengi walichoamua kuiga kwa Haji ni makelele tu. Wanaropoka tu!
Kuna kiburi Haji anawapa mashabiki wa Simba mtaani, matokeo ya hiko kiburi ni mapato kwa klabu.
Baada ya 'Interview' ya leo, nimeelewa kwanini Simba waliamua kuendelea na Haji Manara na kuondoa mpango wa kumuajiri pacha wangu, Gift Macha.
Haji ni 'full package' ya msemaji ambayo haipo tena sokoni.

Haji Manara aliuchukua ujumbe huo na kuuweka kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuibua mijadala  kwa mashabiki wa msemaji huyo.

Post a Comment

0 Comments