BETI NASI UTAJIRIKE

KUELEKEA DERBY: HUYU NDIYE ALIYEBUNI BASI JIPYA LA KLABU YA SIMBA

Baadhi ya wadau wa klabu ya Simba walifurahishwa na picha za basi jipya zilizosambaa mitandaoni siku chache zilizopita lakini hawakufanikiwa kujua mbunifu wakeMbunifu wa basi la Simba anafahamika kwa jina la  Kareem Saidi au maarufu kwa jina la Kareem Designs. Kwa wamiliki wa mabasi yaendayo mikoani jina la Kareem Designs sio geni kabisa kwani ameshafanya  design za rangi kwa mabasi zaidi ya 36.

Msanifu huyu wa rangi za mabasi ameshafanya kazi na makampuni kama Lakrome,Happy Nation,Extra Luxury,Hai  Express ,Sky Line , Kibo EXpress ,Laviha luxury,Kandahar na mengine mengi.

Kwa sasa huhitaji kwenda China kwa ajili ya ubunifu wa mabasi hasa muonekano wa nje na wa ndani, Unachopaswa kufanya ni kuwasiliana na mbunifu huyo na yeye atakupa kila kitu chenye ubunifu wa hali ya juu.

Hii ni baadhi ya kazi zilizofanywa na mbunifu Kareem Said maarufu kama Kareem Designs 
Hivi karibuni nitakuletea makala kamili za mbunifu Kareem Designs ila kwa sasa unaweza tembelea kurasa zake za Instagram kareem_designs_projects

Post a Comment

0 Comments