Kocha Mpya wa Yanga Luc Eymael kesho jumatano ataanza kazi rasmi majukumu ya kuiongoza Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar Mchezo huo
utapigwa katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam . Eymaer alianza kukinoa kikosi cha Yanga hapo jana baada ya kusaini kandarasi ya miezi 18 na klabu hiyo.
Kocha huyo aliyewahi kuipa AS Vita ubingwa wa ligi kuu ya DR Congo ametamba kuwa kikosi chake kina wachezaji wenye vipaji
Inaelezwa tayari vibali vyake vya kukufanya kazi nchini vimepatikana hivyo huenda kesho akakaa kwenye benchi kuwaongoza vijana wake katika mchezo wake wa kwanza
0 Comments