BETI NASI UTAJIRIKE

SVEN APAGAWISHWA NA MAMBO YA KICHUYA ,GEMU NA MWADUI KUANZA

Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji Sven Vandenbroeck amonekana kuvutiwa na kiwango cha Shiza Kichuya aliyeanza mazoezi jana baada ya kurejeshwa Simba katika usajili wa dirisha dogo


Kurejea kwa Kichuya kumeonekana pia kuleta furaha kwa Wanamsimbazi ambao jana walijitokeza kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena kumshughudia nyota wao huyo
Licha ya kutopata nafasi ya kumsogelea kulingana na masharti yaliowekwa na kocha Sven, lakini mashabiki waliojitokeza walionekana kuliimba jina la Kichuya kuonesha jinsi gani wanamkubali mpiga kona wao mahiri.
Mbali na kuwa kivutio kwa mashabiki, Kichuya alionekana pia kupokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake waliompa mkono na kumkumbatia kabla ya kuanza kwa mazoezi hayo.
Baada ya kusalimiana na wachezaji wenzake, Kichuya alipelekwa kwa kocha Sven kutambulishwa , kisha akamtaka kukimbia kwa kuzunguka uwanja kabla ya kujumuika na wenzake katika mazoezi ya pamoja.
Katika mazoezi hayo, yaliyoanza saa tatu asubuhi na kumalizika saa sita, kocha alitoa programu ya mazoezi ya viungo,  kabla ya kuwataka wapige mashuti ya mbali na hatimaye kuwagawa makundi mawili kucheza mechi.
Mara kwa mara Svan alionekana akimuelekeza Kichuya kufanya jambo,  lakini pia akimfuatilia kwa ukaribu kile anachokifanya.
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu, amesema Kichuya ameungana na wenzake, baada ya taratibu za kujiunga na timu hiyo kukamilika.

"Kichuya amejiunga na wenzake leo mazoezini na atakuwa katika kambi yetu ya kudumu  Ndege Beach kwa ajili ya mechi yetu ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Mwadui FC Jumamosi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

"Bila shaka kama atakwenda vizuri na programu za kocha Kichuya anaweza kupata nafasi katika mchezo wa FA kwa sababu ni miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa na Simba"

Post a Comment

0 Comments