BETI NASI UTAJIRIKE

KOCHA LUC EYMAEL ATOA MASHARTI MAKALI KWA WACHEZAJI YANGA

Siku chache baada ya Kocha mpya wa Yanga, Luc Eymael kuanza kibarua katika kikosi amewakataza wachezaji wake kutotumia usafiri wa pikipiki kwa lengo la kuwahi mazoezi .Eymael ambaye alianza majukumu yake Yanga vibaya kwa kuishuhudia timu yake ikichapwa mabao 3-0 na Kagera Sugar jana, amesema wachezaji wote wanatakiwa kutumia basi la klabu hiyo, wakati wa kwenda mazoezini . 

Eymael alisema wachezaji wanapokuwa hawapo kambini watakiwa kufika klabuni mapema ili waweze kuondoka kwa pamoja, lakini si kupanda pikipiki.

"Usafiri wa basi la klabu ni salama zaidi kuliko kutumia usafiri wa pikipiki pia itasaidia wote kufika kwa wakati mazoezini,” alisema Eymael.

Eymael ametua katika klabu hiyo kuchukua nafasi ya Kocha Mwinyi Zahera aliyetimuliwa mwaka jana, baada ya Yanga kutolewa katika michuano ya Kombe la Afrika.

Post a Comment

0 Comments