Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi KMC, ambaye pia ni Meya wa Wilaya ya Kinondoni, Samweli Sitta amesema kuwa walimuajiri Haruna Harerimana baada ya kuwathibitishia kwamba hana mkataba na timu yoyote.
Harerimana ameibukia KMC akitokea Lipuli ya Iringa ambayo imesema kuwa imeamua kumshitaki kocha huyo kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuacha kuifundisha timu hiyo kinyume na mkataba.
Sitta amesema:" Alituthibitishia yeye mwenyewe kwamba hana mkataba na alikuwa ni miongoni mwa wale walioomba kazi baada ya kutangaza nafasi za kazi ndani ya KMC.
Harerimana amesema kuwa:'Unajua Lipuli wamevunja mkataba wao wenyewe kwa miezi saba ambayo nimetumikia wao wamenilipa miezi miwili tu na ushahidi ninao.
Kaimu mwenyeki wa timu ya Lipuli, Ayubu Kihwelo amesema kuwa tayari wamandika barua kutokana na kocha huyo kuonekana katika benchi ya ufundi la KMC kinyume na utaratibu.
“Tumemuandikia barua yeye lakini pia na TFF kwa ajili ya kumfungulia mashataka kwa sababu ameenda kusaini sehemu nyingine akiwa na mkataba halali na Lipuli na mkataba huu ulikuwa unaisha mwezi wa saba ambao ulikuwa wa mwaka mmoja” Kihwelo.
KMC imeingia makubaliano na Harerimana kwa kandarasi ya miezi 18 akichukua mikoba ya Jakson Mayanja.
0 Comments