BETI NASI UTAJIRIKE

HAYA HAPA MAKOSA MANNE YA YANGA WALIYOKUTWA NA BODI YA LIGI (TFF)

Bodi ya Ligi chini TFF iayosimamia kamati ya masaa 72 leo imetoa hukumu kwa kila timu iliyofanya makosa mbali mbali. Klabu ya Yanga imekuwa muhanga wa kamati hiyo baada ya kupewa adhabu 4 peke yao.



Yanga wamekutwa na makosa manne na wanatakiwa kulipa kiasi cha milioni 1,200,000 huku wakipewa onyo kali na tff kuhusu mwenendo wa kocha wao Luc Eymael. Hizi hapa adhabu nne kwa Yanga 

 Adhabu ya kwanza 
Klabu ya Yanga Sc imetozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kurusha chupa za maji kuelekea uwanjani na pia wakati wa mapumzikokwenye mchezo dhidi ya Simba uliopigwa Januari 04 2020.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Kamati ya TFF ya saa 72, mashabiki hao pia waliwarushia chupa za maji waamuzi wakati wanaelekea vyumbani katika mechi hiyo iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Adhabu ya pili
Vile vile katika mchezo huo Klabu ya Yanga Sc imepigwa Faini ya Tsh.200,000/=(Laki Mbili) kwa kutokutumia chumba rasmi kilichoandaliwa kwa kubadilishia nguo.Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo

Adhabu ya tatu
Klabu ya Tanzania Prisons na Yanga Sc zimepigwa Faini ya Tsh.500,000/=(Laki Tano) kila mmoja kwa kosa la kutokuwakilisha vikosi vya timu zao kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo katika mechi hiyo iliyochezwa Disemba 29,2019 katika Uwanja wa Samora mjini Iringa.
Adhabu dhidi ya Timu hizo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.


Adhabu ya nne
Kocha wa Klabu ya Yanga amepewa Onyo kwa kufanya vitendo na kutoa matamshi yasiyofaa na Klabu ya Yanga imeelekezwa kumuelimisha kocha wao na kusimamia nidhamu kwa ujumla..

Post a Comment

0 Comments