BETI NASI UTAJIRIKE

KLABU YA KRC GENK YAMUAGA KWA HESHIMA MBWANA SAMATA

Klabu ya KRC Genk imempongeza na kumuaga Straika Mtanzania Mbwana Samatta aliyesajiliwa rasmi na klabu ya Aston Villa kwa dau la Euro milioni 10. Samatta ameandika


historia ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza ligi kuu Uingereza . Kupitia ukurasa zake za mitandao ya kijamii klabu hiyo iliandika 

"Ulikuja kama kijana wa kawaida, lakini sasa unaondoka kwa heshima kupitia lango kuu ukiwa kama gwiji. 
Tunalia kwakuwa unatuacha lakini tunajivuna na kuona fahari kwakuwa tumekushuhudia ukiwa umevaa jezi yetu kwa kipindi cha miaka minne.
Wewe ni mmoja kati ya watu wakubwa na wa maana sana katika historia ya Genk" -
Post a Comment

0 Comments