BETI NASI UTAJIRIKE

NIYONZIMA AFUNGUKA MIPANGO YAKE NDANI YA YANGA

Kiungo wa Yanga, Mnyarwanda Haruna Niyonzima amesema anatamani kufanya kazi itakayokuwa mfano wa kuigwa na wengine kujituma kwa bidii kuhakikisha wanatwaa ubingwa msimu huu.


Ameweka wazi mikakati yake baada ya kurejea kwa mara nyingine ndani ya klabu hiyo kwamba ni uwezo wake kuonekana zaidi utakaowathibitishia mashabiki kwamba kaja kufanya kazi.

Niyonzima alijiunga na Yanga msimu wa 2011/17 na kuhamia Simba 2017/19 kisha alienda A.S Kigali ya Rwanda na sasa yupo na Yanga, ambapo anataka kujiandikia rekodi Ligi Kuu Bara.

"Natamani uwezo wangu uzungumze zaidi kuliko maneno, naamini mashabiki wanatamani kuona matendo na sio maneno na kama unavyojua soka linachezwa sehemu ya wazi,".
"Kurejea kwangu kuwe kwa manufaa kwa timu, hilo linanifanya niendelee kujituma na kupambana ingawa huwa nafurahia kazi hiyo kwani ipo kwenye damu hivyo sioni kama inanipa wakati mgumu,"amesema.
Kinachomwaminisha Niyonzima ni kufahamu vizuri ligi ya nchini inahitaji nini, jambo linalomrahisishia kazi kuona hakuna linaloshindikana kutimiza.
"Natamani kuwa miongoni mwa wachezaji watakaofanya vyema msimu huu, hilo linawezekana kikubwa uzima ili kuweza kuyaishi ninayofikiria kuyafanya kwani ligi naijua,"amesema.

Post a Comment

0 Comments